HabariMombasaNews

SHULE YA UPILI YA WASICHANA YA MAMA NGINA YAFUNGWA BAADA YA WANAFUNZI WA SHULE HIYO KUJARIBU KUITEKETEZA MOTO ALFAJIRI YA KUAMKIA LEO.

Shule ya upili ya wasichana ya Mama Ngina imefungwa baada ya wanagunzi wa shule hiyo kujaribu kuiteketeza moto alfajiri ya kuamkia leo .
Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Mombasa Peter Magiri amethibitisha kuwa moto ulizuka katika sehemu moja wapo ya kutawadha shuleni hiyo wakati wanafunzi walipokuwa wanajitayrisha kwa masomo yao ya mapema .
Amesema kuwa wasichana wamerudishwa nyumbani huku uchunguzi wa kina kubaini kisa hicho ukianzishwa.
Kwa upande wao wazazi wameulaumu usimamizi wa shule hiyo kwa kutotoa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo
Mama Ngina ndio shule pekee ya kitaifa ya wasichana iliyoko katika kaunti ya Mombasa.

BY NEWSDESK