HabariNews

MSHUKIWA WA ULANGUZI AFUNGWA MIAKA 30 GEREZANI HUKO MALINDI BAADA YA KUKIRI MASHTAKA HAYO.

Mahakama ya malindi imemfunga jamaa mmoja miaka 30 gerezani baada ya kukubali kosa la ulanguzi watu bila kibali.

Abubakar Amin Habib alikubali shtaka hilo la kupatikana akisafirisha raia saba wa taifa la Somali kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab hadi humu nchini.

Awali kiongozi wa mashtaka katika koti hiyo Agatha Ngotho aliambia mahakama kuwa Abubakar akiwa na wmwenzake Jilani Mihadhi ambaye alikataa mashtaka walikamatwa na maafisa wa usalama katika kivuko cha Sabaki kilichoko kaunti ndogo ya Magarini mnamo tarehe 26 mwezi uliopita wakitumia gari dogo aina ya Probox.

Ngotho anasema maafisa wa usalama walipowauliza wawili hao walishindwa kueleza kama wametoka wapi na wanaenda wapi ndiposa wakawatia nguvuni na kuwafungulia mashtaka.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Elizabeth Usui amesema hukumu hiyo inafaa kutoa onyo kwa wote walio na tabia ya kutekeleza ulanguzi wa binadamu.

BY NEWSDESK