HabariNews

Kuna haja kwa sheria za umiliki wa mashamba hasa katika mkoa wa Pwani kufanyiwa marekebisho.

Kuna haja kwa sheria za umiliki wa mashamba humu nchini hasa katika mkoa wa Pwani kufanyiwa marekebisho na kuhakikisha zinapewa nguvu zaidi ili kupunguza unyanyasaji unaoshuhudiwa.
Kulingana na Mwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kilifi Kusini Nicholus Mrima Nyepe, ni kwamba unyanyasaji na uporaji wa ardhi kutoka kwa mabwenyenye kumesababishwa na sharia za umiliki wa mashamba kutofuatwa vilivyo pamoja na sheria hizo kuwa hafifu huku kupelekea wakaazi wengi kufurushwa kutoka kwa makaazi yao kila uchao.
Wakati uo huo, Nyepe amepinga vikali sheria iliyopitishwa ya kuipatia ruhusa serikali ya Kitaifa kutoa amri ya kuchukuliwa kwa ardhi endapo mtu anaishi bila hati miliki huku akitoa wito kwa sheria hiyo kutolewa kupitia kwa kiongozi yeyote atakayeingia madarakani mwaka 2022.

BY NEWSDESK