AfyaHabariLifestyle

WAKENYA WASALIA NA SIKU NANE PEKEE KUHAKIKISHA WANAPATA CHANJO KABLA YA KUKOSA HUDUMA MUHIMU ZA SERIKALI.

Wakenya wana siku 8 pekee kuhakikisha wanapata chanjo la sivyo wakose huduma muhimu za serikali.
Agizo la serikali la utoaji huduma kwa waliochanjwa pekee lilitolewa na waziri wa afya humu Nchini Mutahi Kagwe na linatarajiwa kuanza kutekelezwa tarehe 21 mwezi huu.
Kwa mujibu wa waziri huyo hatua hiyo imechukuliwa ili kuwalinda raia hasa wanapotangamana katika ofisi za serikali, huku idadi ya wanaojitokeza kupata chanjo hiyo kuzidi kuwa chini mno licha ya juhudi za serikali kuhakikisha wakenya wanaipata kwa uraisi.
Kwa mfano wakati wa azimio la umoja katika kaunti ya Nairobi eneo la kasarani, serikali ya Nairobi iliweka kituo cha kutoa chanjo sawa na wakati wa maadhimisho ya siku ya Jamuhuri.
Aidha vituo hivyo vilitembelewa na watu wachache na kufikia sasa ni aslimia 11 pekee ya wakenya waliochanjwa kikamilifu.

BY NEWSDESK