HabariKimataifaNewsSiasa

JESHI LA UGANDA LAKITA KAMBI NJE YA NYUMBA YA BOBI WINE KABLA YA KAMPENI.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ametuma picha ya polisi na jeshi wakionekana nje ya nyumba yake kabla ya kampeni za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kayunga.
Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kutembelea katika wilaya ya Kayunga kumfanyia kampeni mgombea wa chama tawala anayewania nafasi ya uenyekiti.
Uchaguzi huo mdogo umepangwa kufanyika Alhamisi na chama tawala na upinzani kwa pamoja vinataka kuonyesha uwezo wao katika eneo hilo.
Bobi Wine ameshutumu jeshi na polisi kwa kujaribu kumzuwia kuondoka nyumbani kwake.
Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa polisi na jeshi pia wamepelekwaKayunga kabla ya kampeni za Jumanne.

BY NEWSDESK