HabariMazingiraNewsWorld

: Meli ya mizigo yazama Madagascar, yaua zaidi ya 17, makumi ya wengine hawajulikani waliko

Meli ya mizigo iliyokuwa imebeba abiria 130 kinyume cha sheria, imezama katika pwani ya kaskazini-mashariki mwa Madagascar na kuua takriban watu 17 huku wengine 68 wakiwa hawajulikani waliko.
Ripoti kutoka Shirika la Bandari la Madagascar imesema kuwa, takriban watu 45 wameokolewa kutoka kwenye maji ya Bahari ya Hindi.
Meli hiyo kwa jina Francia, iliondoka katika mji wa Antanambe mashariki mwa wilaya ya Mananara Kaskazini mapema Jumatatu na kuelekea kusini kwenye bandari ya Soanierana Ivongo.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika, Jean Edmond amesema chombo hicho kimesajiliwa kama meli ya mizigo, hivyo hakijaidhinishwa kubeba abiria, na Antanambe si bandari rasmi.
Inaaminika kuwa, tundu lililokuwa kwenye sehemu ya meli hiyo ndiyo lililosababisha kuzama kwake.
Madagascar ni kisiwa cha nne kwa ukubwa duniani.