HabariNewsSiasa

Rais Uhuru Kenyatta akagua miradi mbalimbali ya ujezi wa barabara na ukarabati.

Rais Uhuru Kenyatta amekagua miradi mbalimbali ya ujezi wa barabara na ukarabati unaoendelea jijini Nairobi.
Akizungumza katika bustani la Uhuru Park Rais Kenyatta amesema kwamba jiji la Nairobi limeimarika na kuongeza hadhi yake katika ngazi za kimataifa kutokana na mpango wa kuboresha mitaa ya mabanda kama vile Mkuru kwa Njenga miongoni mwa miradi mingine.
Aidha rais amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo mpango wa huduma za afya kwa wote UHC, licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali kama vile janga la corona huku rais akiwakashifu vikali wale wanakosoa utendaji wa serikali yake akisema kuwa serikali haitayumbishwa katika kufanikisha ajenda zake.

BY NEWSDESK