HabariNews

MAAFISA WA POLISI WANACHUNGUZA KISA CHA WATU 6 WALIOUWAWA NA NYUMBA KADHAA KUTEKETEZWA KAUNTI YA LAMU USIKU WA KUAMKIA LEO.

Maafisa wa Polisi wanachunguza kisa ambapo watu 6 wameripotiwa kuuawa na nyumba kadhaa kuteketezwa na watu wanaoaminika kuwa wanamgambo wa Al- Shabab, eneo la widhu Majambeni katika Kaunti ya Lamu usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na wenyeji wa eneo hilo ni kwamba shambulio hilo limefanyika muda wa saa nane alfajiri huku wahalifu hao wakitumia mapanga na silaha hatari ikiwemo bunduki kutekeleza kisa hicho na kuwaacha sita hao wakiwa wameaga dunia na wengine kadhaa kujeruhia vibaya .
Kamanda wa polisi kaunti ya lamu Moses Murithi amethibitisha mauaji hayo kusema kuwa idara ya usalama inaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama kweli mauaji hayo yametekelezwa na wanamgambo au la.
Aidha ameongeza kuwa kufikia sasa bado idadi kamili ya waliouawa na kujeruhiwa haijajulikana huku akiwaomba wenyeji kuwa na subra akidai kuwa serikali tayari imeweka mikakati ya kuimarisha usalama katika maeneo hayo.
Haya yanajiri mwezi mmoja tu baada ya watu 11 kuuwawa katika mashambulizi kama hayo kufanyika katika eneo la Dogogicha na Laaqi kaunti ya Marsabit.

BY NEWSDESK