HabariMombasaNewsSiasa

Pwani si ngome ya ODM asema mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Miraj Abdillahi.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa hususan wanaowanaia nyadhfa mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti wanaendelea kujipigia debe ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi.
Vigogo wakuu ambao wametangaza kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais ni naibu wa rais William Ruto wa chama cha UDA kinara wa ODM Raila Odinga huku muungano wa OKA ukionekana kuyumba kutokana na tetesi za kinara wa ANC Musalia Mudavadi kujiunga na UDA.
Mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Miraj Abdillahi amepuuzilia mbali dhana ya kwamba ukanda wa Pwani ni ngome ya ODM akisema kwamba wakaazi wengi wamejitokeza kujisajili kuwa wanachama wa chama cha UDA.
Miraj vilevile amezungumzia suala la uchumi samawati maarufu Blue Economy akisema kwamba ni jambo la kusikitisha kuona jamii ya wapwani ikiiishi maisha ya kimaskini licha ya bara hindi kuwepo.
Akipigia mfano jamii zingine katika mataifa mengine, Miraj amesema kuwa jamii hizo huishi maisha mazuri na ya juu kutokana na uwepo wa bahari.

BY EDITORIALDESK