HabariNews

Washukiwa kumi wa ugaidi kufikishwa katika mahakama ya Mpeketoni kaunti ya Lamu.

Washukiwa kumi wa ugaidi wanatrajiwa kufikishwa katika mahakama ya Mpeketoni kaunti ya Lamu kwa tuhuma za ugaidi baada ya kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.
Washukiwa hao walikamatwa Jumanne siku moja tu baada ya mauaji kufanyika katika eneo la Lamu Mashariki.
Haya yanajiri huku
Viongozi wa kidini kaunti ya Lamu wameitaka serikali kupitia idara ya upelelezi DCI kufanya uchunguzi wa kina na kubaini wahusika wa mauwaji yaliyotokea katika vijiji vya Widhu-Majembeni na Bobo katika kaunti hiyo.
Mwenyekiti wa maswala ya uwiano wa kidini kaunti ya Lamu Mohamed Abdulkadir amesema haifai kwa maafisa wa serikali kutoa taarifa za kukanganya kuhusu mauwaji hayo akisema kuwa baadhi ya watu wanahusisha mauwaji hayo na mizozo ya mashamba huku wengine wakisema ni mauwaji ya kigaidi.
Abdulkadir amesema serikali inapaswa kutafuta suluhu la kudumu kwa visa vya mauwaji katika kaunti ya Lamu kwani vinaleta athari mbaya kwa uchumi wa kaunti hiyo na hali ya maisha ya wakaazi kwa ujumla.
Aidha amesema itakuwa vyema kwa serikali kuwasajili watu wote wanaoishi na kufanya shughuli zao sehemu za mashambani ili kujua wanatoka wapi na wanajihusisha na kazi gani katika maeneo hayo.
Amesema hii itasaidia katika kufautilia na kujua ni watu gani wanaohusika na visa vya uhalifu pindi visa hivyo vinapotokea.

BY EDITORIAL DESK