HabariNewsSiasa

Jaji mkuu Martha Koome anatarajiwa kuliongoza jopo la majaji saba watakaosikiliza kesi ya mswaada wa BBI

Jaji mkuu Martha Koome anatarajiwa kuliongoza jopo la majaji saba watakaosikiliza kesi ya mswaada wa kuifanyia katiba marekebisho BBI hapo kesho.
Kesi hiyo itasikizwa kwa siku tatu ambapo ni kuanzia hapo kesho hadi Alhamisi.
Kulingana na mwongozo uliotolewa na mahakama mwaka jana ni kwamba wahusika wakuu akiwemo mwanasheria mkuu Paul Kihara na Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC watapewa takriban dakika 45 kila upande kuteteta hoja zao huku wahusika wengine wakipewa takriban dakika 15.