HabariNews

HATIMAYE MFANYIBIASHARA JIMMY WANJIGI AFIKISHWA MBELE YA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MILIMANI JIJINI NAIROBI.

Hatimaye Mfanyibiashara Jimmy Wanjigi amefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani Benard Ochoi. Upande wa Mashtaka umependekeza mashtaka sita dhidi ya mfanyibiashara huyo yakiwemo ya kushirikiana na wau wengine kutekeleza uhalifu, kughushi cheti cha umiliki wa Ardhi katika eneo la Westlands Jijini Nairobi miongoni mwa mengine. Wakili wa Wanjigi aidha amelalamikia kukamatwa kwa mteja wake licha ya Mahakama Kuu kutoa agizo la kuzuia kukamatwa kwake akisema kwamba hatua hiyo ni ukiukaji mkubwa wa maagizo ya Mahakama. Wengine walioshtakiwa nae ni pamoja na mkewe Irene Nzisa japo hajawasilishwa Mahakamani.