HabariNewsScience

Takriban watu 265 wamefariki katika ajali tofauti za barabarani humu nchini tangu Mwezi Januari mosi 1, mwaka huu.

Takriban watu 265 wamefariki katika ajali tofauti za barabarani humu nchini tangu Mwezi Januari mosi 1, mwaka huu.
Hili ni ongezeko la asilimia 32 ya matukio kama hayo ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Kamanda wa trafiki jijini Nairobi Mary Omari amesema kwamba takriban watu 201 walifariki kutokana na ajali katika kipindi kama hiki mwaka jana.
Watembea kwa miguu wamechangia vifo vingi, huku Kaunti ya Nairobi ikiongoza kwa waathiriwa 85, ikifuatiwa na eneo la Magharibi ambalo linaongoza kwa ajali za pikipiki.
Zaidi ya watu 400 aidha, wanauguza majeraha nchini kutokana na ajali tofauti huku kulingana na polisi ni kwamba uendeshaji wa magari na pikipiki kwa kasi ndio chanzo kikuu cha ajali za barabarani.