HabariNews

Mzozo kati ya Serikali ya Kaunti ya Kilifi na kampuni ya ukusanyaji ushuru ya Rains drops Limited unazidi kutokota.

Mzozo kati ya Serikali ya Kaunti ya Kilifi na kampuni ya ukusanyaji ushuru ya Rains drops Limited, unazidi kutokota baada ya Serikali ya Kaunti kubatilisha mkataba wa kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo Shaid Mgambi ni kwamba kampuni hiyo imepata amri ya mahakama kuitaka kurejea kazini siku moja baada ya kutimuliwa na serikali ya kaunti ya kilifi.
Itakumbukwa kwamba Serikali ya Kaunti ya Kilifi ilikuwa imetoa ilani kwa vyombo vya habari kuitaka kampuni hiyo kusitisha mara moja ukusanyaji wa ushuru kwa niaba yake.