HabariNewsSiasaWorld

Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini IEBC imeanza kuwasajili wakenya walioko ng’ambo.

Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini IEBC imeanza kuwasajili wakenya walioko ng’ambo hii leo na kutarajiwa kutamatika Februari 6.
Kando na Mataifa mengine yaliokuwa yakipiga kura, Tume hiyo imeongeza Mataifa mengine ya ughaibuni kwenye orodha yake ikiwemo Mataifa ya Uingereza, Canada, Marekani, Sudan Kusini, Milki za falme za kiarabu na Ujerumani.
Tume ya IEBC aidha, inalenga kujaza pengo la watu milioni 4.5 waliokosa kujisajili katika awamu ya kwanza ambapo tume hiyo ilikuwa imelenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni 6 kufikia mwishoni mwa zoezi hilo katika awamu ya kwanza.
Wakati uo huo raia wa Kenya wanaoishi katika Mataifa ya Burundi, Tanzania, Rwanda, Uganda na Afrika kusini wana nafasi ya kujisajili kama wapiga kura kwenye afisi za ubalozi wa mataifa hayo.