HabariMazingiraNews

Asilimia 90 ya vyanzo vya maji katika eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale vimekauka kufatia kiangazi.

Asilimia 90 ya vyanzo vya maji katika eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale vimekauka kufatia kiangazi ambacho kimeshuhudiwa kwa muda mrefu sasa na vijiji vilivyoathriwa zaidi ni Soloita, Mikanini, Kalwembe na Vukato.
Mvua chache iliyonyesha mwezi disemba mwaka uliopita haikusaida kwani vyanzo vichache vilivyosalia vinaendelea kukauka hali inayowaweka wanafunzi katika hatari ya kususia masomo na kulazimika kuwasaidia wazazi kutafuta maji kwa matumizi nyumbani.
Mwaka uliopita ukame ulisababisha asilimia kubwa ya mifugo katika maeneo mbalimbali ya Kwale kufa hali inayotarajiwa kushuhudiwa tena hivi karibuni.
Wakaazi wa eneo hili wamekuwa wakitembea takriban kilomota 20 kutafuta maji kwenye mto umba na wanaendelea kuomba msaada wa maji na chakula kwao na hata kwa mifugo wao.