Agnes Mjd almaarufu Agnes leisch Alizaliwa na kukulia Kibwezi nchini Kenya. Agnes Mjd alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 10 kuwaburudisha wanafunzi wenzake shuleni. kujitosa katika taaluma mnamo Novemba 2014 kama msanii salama alitoa nyimbo 8. Kufikia Machi 2019 aliamua kuokoka na kuanza rasmi mziki wa Injili hatua ambayo haikuchukuliwa vizuri na baadhi ya mashabiki wake.
“Nilihisi kuhukumiwa, kutengwa na kutostahili katika Jamii. Wakati huo niligundua wokovu sio kutembea kwenye bustani, unahitaji mawe mengi na dhabihu lakini Mungu ni mwingi wa Rehema. Nilijua hata kabla sijaanza muziki wa kidunia ipo siku nitarudi kwenye muziki wa injili coz huko ndiko nilikozaliwa” Agnes Mjd akulia na kulelewa katika Familia ya Kikristo, Babu yake alikuwa mchungaji, kulingana na Agnes alikua anasubiri muda muafaka wa kuhudumu.Agnes ambaye kwa sasa anaishi Ujerumani alitoa ngoma kwa jina watangoja sana, ngoma iliomtambulisha rasmi kwenye mziki wa Injili.
Kwa sasa anaishi Ujerumani, kando na kuimba yeye ni mama wa watoto 2.Kufikia sasa Agnes amefanikiwa kutoa Album moja na anatarajiwa kuachilia ngoma nyengine mpya 29,01,2022 kwa jina ‘Msalaba’
Tizama moja kati ya kazi zake hapa.
By Yussuf Tsuma