HabariLifestyleNews

Serikali imetakiwa kubuni vituo vya kutoa ushauri nasaha na mafunzo ya kidini katika ngazi za kaunti kote nchini ili kupunguza visa vya maafisa wa polisi kujitoa uhai.

Serikali imetakiwa kubuni vituo vya kutoa ushauri nasaha na mafunzo ya kidini katika ngazi za kaunti kote nchini ili kupunguza visa vya maafisa wa polisi kujitoa uhai haya ni kwa mujibu wa afisa aliyestaafu eneo la Pokot Magharibi John Arile.
Kulingana na OCPD wa Mvita kaunti ya Mombasa pendekezo hili litachangia pakubwa kukomesha visa hivi humu nchini huku akiwataka maafisa kuweka wazi changamoto zao ili waweze kupata usaidizi. Maoni sawia na haya yametolewa na Dorica Chebet ambaye ni mwanasaikolojia, amesema wengi wa maafisa wa polisi huokosa kuweka wazi changamoto zao kutokana na kasumba kadhaa miongoni mwa wanajamii.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na Tume ya Huduma ya Kitaifa za Polisi (NPSC) wiki jana jumla ya maafisa 12,000 wanakabiliwa na matatizo haya huku afisa mkuu mtendaji wa NPSC Johseph Onyango akisema takwimu hizi zinaakisi hali ya changamoto ya maafisa nchini.

BY EDITORIAL DESK