AfyaHabariLifestyleNews

Idara ya usalama katika kaunti ya Mombasa imewataka vijana kuacha kutumia dawa za kulevya.

Idara ya usalama katika kaunti ya mombasa imewashauri vijana kujitenga mbali na matumizi ya dawa za kulenya.Mkuu wa polisi eneo la Mvita katika kaunti ya Mombasa Joseph Ongaya amesema kwamba matumizi ya mihadarati yamekua na athari kubwa katika afya na maisha ya vijana hao kwa jumla.
Kwa upande wake Abbas Matata, kijana kutoka eneo la likoni ambaye ameamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya, amekiri kupata hasara kubwa kwa takriban miaka 10 ya kutumia mihadarati hiyo.
Matata amewasihi baadhi ya vijana ambao wangali kutumia dawa za kulevya kujitahidi na kujinasua kwa faida yao wenyewe.

BY EDITORIAL DESK