HabariSiasa

BARAZA LA MAKANISA LAANZISHA KAMPENI ZA AMANI KAUNTI YA KWALE…………

Baraza la makanisa nchini NCCK limeanzisha kampeni za amani kaunti ya Kwale ili kuona kuwa jamii zinaishi na uwiano na utangamano kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi wa Agosti.

Kulingana Janeglory Gichane muchungaji wa kanisa la Free Pentecostal Church of kenya kampeni za misingi ya ukabila zinazoshuhudiwa katika kaunti hiyo huenda zikaleta mihemko na migawanyiko.

Ameisitizia kuwa jamii zisigawanyike katika misingi ya aina yeyote badala yake kusubiri siku ya uchaguzi na kutimiza haki zao za kikatiba.

By Yussuf Tsuma