Taasisi ya utafiti wa matibabu nchini KEMRI imezindua kifaa cha kunakili na kurekodi habari muhimu za mama na mtoto baada ya kujifungua.
Naibu mkurugenzi wa mawasiliano katika taasisi hiyo David Mkoji amesema kuwa kifaa hicho kitatumika kunakili alama za vidole, uso na sauti ya mama pamoja na mtoto aliyezaliwa.
Kulingana na mkoji, kifaa hicho kinalenga kuboresha utoaji wa chanjo na huduma za matibabu kwa mtoto kila wakati mama anapotembelea hspitali.
Kwa upande wake mshirikishi wa mradi huo Rukia Hassan amebainisha kuwa kwa sasa wanafanya majaribio katika hospitali ya Kinango.
Hassan amesema kwamba mradi huo unaotekelezwa na chuo kikuu cha Nagasiki kwa ushirikiano na shirika la Nipon Electronic Corporation (NEC) unalenga wanawake wanaojifungua katika hospitali hiyo.
>>News desk