HabariMombasaNewsSiasa

Ni jukumu la kila mkaazi wa Mombasa kuwa mstari wa mbele katika kueneza amani.

Kamati ya idara ya usalama hapa mjini Mombasa imewasisitiza wakaazi wake haswa, wa eneo bunge la mvita kudumisha amani ambapo taifa linakaribia uchaguzi mkuu.
Wakiongozwa na naibu kamishna wa eneo la bunge hilo la mvita Ronald Mwiwawi ,katika mkutano uliowaleta pamoja kamati ya usalama ,baraza la wazee pamoja na wenyeji wa eneo bunge hilo, amekariri kuwa ni jukumu la mkaazi wa Mombasa kuwa mstari wa mbele katika kueneza amani na kupinga vikali siasa za vurugu.