HabariMombasa

WAKAAZI ENEO LA TUDOR KAUNTI YA MOMBASA WALALAMIKIA UHABA WA MAJI.

Wakaazi wa swa maeneo ya Tudor na Kaa chonjo kaunti ya Mombasa wanaitaka serikali ya kaunti kushughulikia swala la uhaba wa maji shida ambayo imewatatiza kwa mudaa sasa.
Wakizungumza na meza yetu ya Habari, wakaazi hao wamesema kuwa kukosekana kwa mifereji ya maji safi na bei ghali ya mtungi wa maji kupatikana kumewalazimu baadhi yao kunywa maji ya visima kutokana na bei yake ya chini na kupatikana kwa wingi.
Wameongeza kuwa imewalazimu wengi wao kukinga maji ya mvua kunaponyesha na kutumia maji hayo kunywa na hata wakati mwingine kutumia katika mapishi.
wakaazi hao wanaiomba serikali ya kaunti kutafuta mbinu mbadala ya kusawazisha shida hiyo kwa kujenga mifereji itakayo wawezesha kupata maji safi mitaani kwa urahisi na kwa bei nafuu ili kuepukana na athari za magonjwa kama vile kipindu pindu.

BY EDITORIAL DESK