HabariMombasaNewsSiasaSports

UBABE WA JUMWA NA KINGI KILIFI.

Wafuasi wa gavana wa Kilifi ambaye pia ni kinara wa chama cha PAA amazon Kingi wamemsuta mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kwa kile walichokidai kuwa kumkosea heshima gavana kingi.
Hayo yanajiri huku wawili hao wakizidi kunyesha ubabe wao katika siasa za kaunti ya Kilifi.
Wakiongozwa na Patience Kipusa, wafuasi hao wamesema kuwa wanaheshimu azma ya Jumwa kuwania ugavana Kilifi na hivyo basi asimtusi kiongozi wa PAA Amason Kingi.
Aidha Kipusa amedai kuwa hawafurahishwi na jinsi Jumwa anafanya kampeni zake na kumtaka kuuza sera zake na kuwaachia wanachi uamuzi wao kwenye debe.
Itakumbukwa kwmba, Jumwa alidai kuwa mkataba waliotia saini ni kuwa PAA haingewasilisha wagombea katika kaunti ya Kilifi jambo ambalo Gavana Kingi alipinga na kusema kuwa PAA itawasilisha wagombeaji katika nyadhfa zote isipokuwa tu ile ya urais.