HabariMazingiraNewsSiasa

Tume ya uiano na utengamano Ncic imetaja kaunti ya Mombasa miongoni mwa kaunti ambazo huenda zikashuhudia vurugu.

tume ya uiano na utengamano Ncic imetaja kaunti ya Mombasa miongoni mwa kaunti ambazo huenda zikashuhudia vurugu na machafuko wakati wa uchaguzi mkuu wa agosti tisa.

Kulingana na NCIC kaunti za Nairobi, Kisumu uasin gishu, nakuru na kericho vile vile huenda zikashuhudia vurugu

Kaunti sita zimemulikwa kuhusiana na vurugu zinazotokana na matokeo ya uchaguzi.

Katika Ripoti yake NCIC imesema vurugu hizo huenda zikatokana ukosefu wa usawa kwenye ugawanyaji wa rasilimali, vile vile idadi kubwa ya watu wanaoishi sehemu hizo ambao wanatoa mianya ya makundi ya wahalifu kutekeleza maovu

Akizungumza katika kikao cha kutoa ripoti kuhusu maeneo ambayo yanakisiwa kutokea machafuko, kamishna na NCIC Danvas makori, Amesema hatua ya kwanza ni kwa idara zote muhimu katika mchakato wa uchaguzi kushirikiana.

Makori amesistiza haja ya idara zote kudumisha demokrasia na uwazi kwa mfano katika shughuli ya tume ya uchaguzi ya kuidhinisha wagombeaji.

Makori vile vile amesema vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa katika shughuli nzima.