Muungano wa wachungaji kaunti ya Kwale sasa unaitaka tume ya uchaguzi nchini (IEBC) kuwaagiza wanasiasa kuhubiri amani wakati wanapofanya kampeni zao ili kuzuia machafuko katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti wa muungano huo Askofu Peter Mwero ameitaka tume ya IEBC kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa watakaopatikana wakiwachochea wananchi kuzua vurugu kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Aidha, Mwero pia ameitaka tume hiyo kuwazuia wanasiasa watakaotoa matamshi ya chuki na uchochezi wakati huu wa kampeni kutoshiriki katika uchaguzi wa Agosti 9.
Kwa upande wake mchungaji katika muungano huo Selina Esau umeupigia debe uongozi wa wanawake wanaolenga kupigania nyadhifa mbali mbali za kisiasa nchini.
Haya yanajiri baada ya muungano huo kufanya matembezi ya amani pamoja na maombi maalum katika mji wa Kinango kuliombea taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu.
>> News Desk…