HabariTechnology

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi wa idara ya upelelezi DCI.

Rais Uhuru Kenyatta hii leo anatarajiwa kuongoza uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi wa idara ya upelelezi DCI.
Maabara ya uchunguzi wa DCI ni Kituo cha hadhi ya Kimataifa hasa katika maswala ya kufanya uchunguzi wa kina na Kukabili uhalifu.
Kwa mujibu wa DCI, Kituo hicho kitaongeza uwezo wa kutumia mbinu za kisasa za uchunguzi na sayansi katika utekelezaji sheria.
Wananchi ambao walikuwa wakitaka kuhudumiwa hii leo katika ofisi ya idara ya DCI wamearifiwa kuwa ofisi hiyo imefungwa kwa ajili ya uzinduzi huo wa kituo hicho cha maabara ya DCI.

>> News Desk.