Mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Madola unaanza leo nchini Rwanda huku taifa hilo likichunguzwa kuhusu rekodi yake ya haki za binadamu wakati makubaliano yake ya wahamiaji na Uingereza yakitishia kuangaziwa zaidi katika mkutano huo. Ushindani mkali wa uongozi wa jumuiya hiyo yenye mataifa 54 ambayo ni makoloni ya zamani ya Uingereza pia unafanyika huku jumuiya hiyo ikikabiliana na mabadiliko ya utambulisho wake na umuhimu wake katika siku zijazo. Mwanamfalme Charles, anayemwakilisha Malkia Elizabeth II kama mkuu wa Jumuiya ya Madola, amefanya ziara ya kwanza ya kifalme ya Uingereza nchini Rwanda kwa mkutano huo, ambao unakamilika baada ya siku mbili za mikutano ya uongozi. Mwanamfalme Charles pia anatarajiwa kukutana leo na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pembezoni mwa mkutano huo ambaye amekuwa akipigia debe mpango wake uliokosolewa vikali wa kuwahamisha wahamiaji kuelekea Rwanda tangu alipowasili mjini Kigali hapo jana.
>> News Desk…