HabariKimataifa

Rais Joe Biden amesema Marekani itaweka makao makuu mapya ya kijeshi ya kudumu nchini Poland.

Rais Joe Biden amesema Marekani itaweka makao makuu mapya ya kijeshi ya kudumu nchini Poland na kupeleka vikosi vya ziada vya ardhini, angani na baharini kote barani Ulaya, kujibu vitisho kutoka Urusi.

Biden ametangaza kwenye mkutano wa kilele wa jumuiya ya kujihami NATO, kwamba Marekani itapeleka meli mpya za kijeshi nchini Uhispania, ndege za mapigano nchini Uingereza, wanajeshi wa ardhini nchini Romania, na mifumo ya ulinzi wa angani nchini Ujerumani na italia, na zana nyingine tofauti katika kanda ya Baltic.

Pia ametilia mkazo ahadi ya muungano huo wa kijeshi wa kanda ya Atlantiki kulinda kila nchi ya ardhi yake, na amewaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa mkutano na katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, kwamba shambulio dhidi ya mwanachama yeyote wa NATO ni shambulio dhidi ya wote.

>> Editorial Desk..