HabariNewsSiasa

Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi wa urais

Aliyekuwa mwaniaji wa urais kupitia Azimio la Umoja Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati akisema kuwa si ya saw ana hayazingatii haki.

Akiwahotubia waandishi wa habari katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi Raila amesema kuwa matokeo hayo ni lazima yapingwe kwenye mahakama ya sheria .

Aidha amesema kuwa , hatua ya wafula Chebukati kutumia nguvu katika kutangaaza matokeo hayo na kutoruhusu makamishna wengine wanne kuthibitisha matokeo ya urais ni ishara ya kutokuwa na uwazi katika tume ya IEBC .

Hapo jana Chebukati alimtangaza Ruto kuwa rais mteule baada ya kupata kura 7,176,141 dhidi ya mpinzani wake mkali Raila aliyepata kura 6,942,930 ambayo ni asilimia 48,85 ya jumla ya kura zote zilizopigwa.

Wakati huohuo amewapongeza makamishna waliojitokeza kimasomaso kutetea haki na kudhihirisha ukweli huku akiwaomba kutokuwa na hofu kwani wakenya wote wako Pamoja nao.

BY EDITORIAL TEAM