Waziri wa elimu prof George Magoha amesema tarehe ya kurejelewa rasmi kwa shughuli za elimu itasalia vivyo hivyo yaani kesho tarehe 18.
Shule zimefungwa kwa wiki mbili kupisha maandalizi ya uchaguzi uliofanyika tarehe 9 mwezi huu.
Magoha aidha ameendelea kuwaomba wakenya msamaha kutokana na kauli zake anazosema zilitafsiriwa visivyo akisisitiza kuwa lengo lake ni kuinua sekta ya elimu.
Haya yanajiri huku wazazi wakilazamika kulipa karo kamili licha ya wanafunzi kuchelewa kurudi shule hali ambayo imezidi kuwakandamiza wazazi.
Akizungumza na meza ya habari Alex Wafula mkaazi wa mjini Mombasa amelalamikia swala la karo ya shule kutokana na wanafunzi kukaa kwa muda nyumbani kufuatia changamoto za uchaguzi.
Hata hivyo Wafula ameitaka wizara ya elimu kushughulikia swala la karo ili kuzuia wanafunzi kurundishwa nyumbani kulingana na muhula mfupi wa masomo ikizingatiwa hali ngumu ya kiuchumi humu nchini.
BY EDITORIAL DESK