Idadi ya visa vya mimba za mapema miongoni mwa wasichana wa umri mdogo imetajwa kuongezeka katika ukanda wa pwani kufuatia sababu mbalimbali.
Akizungumza na meza yetu ya habari mkurugenzi mkuu wa shirika la sisters for justice Neila Abdalla amedokeza kuwa umaskini unaokumba familia nyingi na hali ya uchumi inayoshuhudiwa nchini ni sababu kuu zinazochangia kuongezeka kwa idadi ya visa hivi kwani vinawasukuma wasichana wengi kujihusisha na ngono ili kupata pesa za kujikimu kimaisha.
Aidha Neila amewalaumu wazazi kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo huku akiwahimiza kuwa mstari wa mbele kuwashauri na kuwatahadharisha wasichana wao kuhusu athari za kujihusisha na ngono za mapema.
Vilevile mkurugenzi huyo ameeleza kuwa shirika hilo limeweka mikakati kabambe kupigana dhidi ya visa hivyo na kusema kuwa atakeyepatikana akimdhulumu mtoto wa kike atachukuliwa hatua za sheria.
BY EDITORIAL DESK.