Baadhi ya viaana wanaofanya Biashara mtandaoni wamesema njia hio ya biashara imewasaidia vijana wengi katika kujiajiri kwa gharama nafuu wakati huu ambapo taifa linakumbwa na uhaba wa nafasi za ajira na hali ngumu ya maisha.
Katika mahojiani ya kipekee na vijana hao, wamesema kuwa serikali imekuwa ikitoza ada kubwa ya kodi za biashara na hivyo kuwalazimisha kufanya biashara mitandaoni.
Wakiongozwa na Philip bakari mfanya biashara ya kuuza nguo mtandaoni, amesema kuwa biashara hizo zanawasaidia kujiajiri kwa gharama chache hali ambayo imewapa nafasi kufikia soko kubwa la wateja mtandaoni.
Vijana hao wamekemea baadhi ya wafanya biashara ghushi wanaopotosha wateja mtandaoni na kuitaka serikali kujali biashara hizo na kuweka mikakati itakayowakabili walaghai katika biashara hizo.
BY EDITORIAL DESK