Uharibifu wa mali ya umma ikiwemo mabomba ya mifereji umetajwa kuwa kizingiti kikuu ambacho kimesababisha wakaazi wengi katika eneo bunge la Kinango kukosa maji.
Kulingana na chifu wa Puma Saumu Luvuno baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kukata mabomba ya mifereji katika visima ambavyo ni tegemeo kuu kwa wakaazi hatua ambayo imemlazimu kuripoti visa hivyo katika kituo cha polisi cha Kinango.
Ni hatua aliyoitaja ya kutamausha huku akiwaomba wakaazi kuwa mstari ya mbele kulinda raslimali zao.
Hata hivyo Gavana wa Kwale Fatuma Achani amekiri kupokea taarifa hio huku akiwaonya wakaazi kuwa atakayepatikana akiharibu mali ya umma atakabiliwa vilivyo.
Achani amesisitiza kuwa ipo haja ya jamii kulinda miradi inayotekelezwa na serikali ya kaunti kuilinda akisema kuwa serikali yake iko mbioni kuhakikisha uhaba wa maji unazikwa katika kaburi la sahau.
BY EDITORIAL DESK