Tume ya utendakazi wa polisi nchini IPOA imethibitisha kupokea kesi elfu 20 kufikia sasa zinazohusiana na upotofu wa nidhamu miongoni mwa maafisa polisi humu nchini.
Zaidi ya kesi elfu 3 zikifanyiwa uchunguzi huku uchunguzi dhidi ya takriban kesi elfu 4 ukikamilika na kuwasilishwa katika afisi ya DPP.
Dennis Okech msimamizi wa kitengo cha mawasiliano katika tume hio ya IPOA aliyekuwa akizungumza huko Ukunda kaunti ya Kwale katika mkao wa kutathimini jinsi maafisa wa polisi walivyoendesha shughuli zao wakati wa zoezi la uchaguzi mkuu uliopita, amesema kwamba kwamba afisaa wa polisi atayekiuka maadili atakabiliwa kisheria.
Okech amewataka maafisa wa polisi kuzingatia maadili pasi na kukiuka sheria za nchi.
Kwa upande wake Mwalimu Rama afisaa wa nyanjani wa shirika la kijamii la Kecosce aliyeandaa mkao huo kupitia mradi wa Safe Coast amesema kuwa kuna haja ya maafisa wa polisi kudumisha uiayano na jamii ili kuhakikisha usalama unadumishwa nchini.
BY EDITORIAL DESK