Wakaazi wa kaunti ya Kwale wamempongeza rais William Ruto kwa kumteua aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya katika wizara ya madini na uchumi wa baharini.
Wakizungumza baada ya Mvurya kuapishwa kuwa waziri katika wizara hiyo, wakaazi hao wamemtaka waziri huyo mpya kuangazia changamoto zinazoathiri sekta ya madini kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Mrinzi Nyundo, wakaazi hao wamemtaka waziri huyo kuhakikisha kampuni hiyo inawapa kipaumbele wenyeji katika nafasi za ajira.
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea wa kiti cha mwakilishi wa kike kaunti hiyo Bibi Masha amemtaka Mvurya kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa ili kuwafaidisha wakaazi walioathirika na shughuli za uchimbaji madini zinazotekelezwa na kampuni ya Base Titanium.
Haya yanajiri baada ya serikali ya kaunti hiyo kukosa kufaidika na asilimia 30 ya mgao wa fedha za madini ya kampuni hiyo.
BY EDITORIAL TEAM