HabariNews

Hisia mseto zimeibuliwa na wakaazi wa kaunti ya Kwale kuhusiana na utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu (CBC).

Baadhi ya wakaazi wameupinga mtaala huo na badala yake kuitaka serikali kuboresha mfumo wa zamani wa 8-4-4.

Wakiongozwa na Hussein Mgunga, wakaazi hao wamedai kuwa wazazi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama ya utekelezaji wa CBC.

Kwa upande wao wakaazi wanaounga mkono mtaala huo wameitaka serikali ya kitaifa kugharamia elimu ya CBC ili kuwapunguzia wazazi mzigo.

Wakiongozwa na Kevin Olouch, wakaazi hao wamesema kuwa ujio wa CBC unalenga kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo wa zamani.

Wakaazi hao wameyasema hayo katika kikao cha kukusanya maoni ya umma kuhusu mtaala wa CBC kwa jopo maalum lililobuniwa na rais William Ruto.

BY EDITORIAL DESK.