Watu wawili wanaendelea kupokea matibabu katika hosipitali kuu ya makadara baada ya kuvamiwa na kundi la wahalifu asubuhi ya kuamkia leo katika wodi ya mtopanga eneo bunge la kisauni kaunti ya Mombasa.
Akiongea na meza yetu ya habari wakati akipokea matibabu ndani ya hosipitali hiyo mmoja wa wathiriwa amesema kuwa alivamiwa na kundi la vijana 6 na kumkata kata mapanga kabla ya kumpokonya simu na pesa alizokuwa nazo akielekea kazini mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
Dr Sumeiya akidhibitisha tukio hilo amesema kuwa hosipitali ya Coast General imekuwa ikipokea wagonjwa wa kukatwa katwa na mapanga kutoka eneo hilo kati ya siku 3 hadi 5 kila wiki.
Mwakilishi wodi eneo hilo Morgan Matsaki amekemea kitendo hicho na kutaka idara husika kufanya jitihada ili kuweza kuboresha usalama kwani jamii nyingi zimeathirika kutokana na utovu wa usalama unaoshuhudiwa .
Kulingana nae eneo hilo kwa sasa linakabiliwa na ukosefu wa usalama hatua ambayo ameiomba serikali kupitia idara husika kuingilia kati ili kuwanusuru wenyeji.
Tukio hilo linajiri siku chache baada ya maduka kuripotiwa kuvamiwa na wenyeji kuvurugwa na wahuni hao huko mtopanga, wakazi sasa wakitaka jibu kutoka kwa maafisa wa serikali ambao wanasema wamezembea kazini.
BY DAVID OTIENO.