HabariNews

SHIRIKA LA HUDUMA ZA KUSIMAMIA MISITU NCHINI LIMESEMA KUWA MIKAKATI ZAIDI IMEWEKWA ILI KUDHIBITI UKATAJI MIKOKO.

Shirika la Huduma za kusimamia misitu nchini (KFS) limesema kuwa mikakati zaidi imewekwa ili kudhibiti ukataji mikoko katika fuo za bahari nchini.

Akizungumza na meza yetu ya habari mshikadau katika shirika hilo kaunti ya Mombasa Jeremy Mutuku amesema kuwa wanashirikiana na idara mbali mbali nchini ili kudhibiti ukataji misitu katika fuo za bahari hususan mikoko.

Aidha amesema atakayepatikana akikata mikoko basi atachukuliwa hatua kisheria.

Vile vile ameongeza kuwa shirika hilo liko mbioni kupiga jeki mpango wa serikali wa kupanda miti kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali akisema kuwa tayari mpango huo unaendelea kutekelezwa katika fuo za bahari na maeneo mengine nchini katika juhudi za kutunza misitu huku akiwashauri wananchi kushabikia jukumu la upandaji miti.

BY EDITORIAL TEAM