HabariNews

Wakazi wa eneo bunge la kinango watunukiwa chombo cha kusafirisha maji aina ya tuk tuk.

Wakazi wa eneo bunge la kinango wanakila sababu ya kutasamu baada ya usimamizi wa wakfu wa Jefa kuwatunuku na chombo cha kusafiria maji aina ya tuk tuk kitakacho wasaidia katika kusambaza maji wakati huu ambako eneo hilo linashuhudia kiangazi.

Akizungumza na meza yetu ya habari wakati wa kumkabidhi mbunge wa eneo hilo Gonzi rai chombo hicho msimamizi wa wakafu huo Yusuf Njiwa amesema kuwa hatua hiyo imejiri ili kusaidia jamii ambazo tayari zinaathiri na ukosefu wa maji hasa katika kaunti ya kwale na Mombasa.

Ameongeza kuwa mradi huo utaendelea katika kaunti zote za pwani Mombasa na kwale zikiwa a kwanza kunufaika na mpango huo.

Kwa upande wake mbunge wa kinango Gonzi rai amepongeza juhudi za wakfu wa jafar akisema kuwa umekuwa ukisaidia pakubwa jamii zisizojiweza huku akiwahidi wakazi wa eneo hilo kwamba uongozi wake pitia wafadhili mabli mbali utahakikisha kwamba wanapata afueni hasa wakati huu wa kianagazi.

Kuhusu swala njaa ambalo limekithiri katika eneo hilo mbunge huyo amesema kuwa ana mikakti ya kushirikisha wafadhili pamoja na serikali ili kuzidi kutoa msaada ambayo kwa sasa imeanza kutolewa na serikali .

BY EDITORIAL DESK