HabariNews

MAKATIBU WA WIZARA MBALIMBALI WAENDELEA KUHOJIWA NA KAMATI NNE ZA BUNGE BUNGENI.

Mahojiano ya makatibu walioteuliwa kuhudumu katika wizara mbalimbali yanaendelea kwa sasa ambapo yanaendeshwa na kamati nne za bunge.

Katibu mteule wa wizara ya fedha Dkt Chris Kiptoo ambaye amehojiwa na kamati ya uwekezaji na biashara, amesema kuwa anautajiri wa shilingi milioni 338

Kiptoo amesema kuwa ipo haja ya serikali kuweka sera mwafaka ili kubuni njia isiyo ghali ya kufufa biashara na kukusanaya kodi.

Aidha ameeleza kuwa iwapo ataidhinishwa basi atahakikisha kuwa mamlaka ya ukusanyaji kodi KRA inailetea serikali mapato bila kuwaumiza wananchi vilevile ameahidi kuwahusisha washikadau mbalimbali ili kuimarisha mazingira ya kibiashara nchini.

Aidha kwa upande wake Julius Korir ambaye katibu mteule wa idara ya masuala ya wizara mbalimbali ametetea wadhfa huo mbele ya kamati ya utawala na masuala ya ndani ya nchi akisema majukumu yake ni tofauti na yale ya katibu wa baraza la mawaziri.

Korir ametaja kuwa ana utajiri wa shilingi milioni 206.

BY EDITORIAL TEAM