HabariNews

Onyo latolewa na idara ya usalama dhidi ya wahalifu wanaotatiza usalama wa wahudumu wa bodaboda eneo bunge la Shimba Hills.

Onyo latolewa na idara ya usalama dhidi ya wahalifu wanaotatiza usalama wa wahudumu wa bodaboda eneo bunge la Shimba Hills hususan wadi ya mkongani kaunti ya Kwale.

Hii ni baada ya kuripotiwa visa vya wahudumu wa bodaboda kutoka maeneo hayo kupatikana wameuwawa na miili yao kutupwa katika mbuga ya wanyama iliyoko karibu ya Shimba Hills.

Akizungumza eneo la Kizibe naibu kamishna wa eneo bunge hilo Moses Karwigi adokeza kuwa asasi za usalama zinashika doria pia kuchunguza na kuwasaka wahalifu wanaohusika katika visa hivyo vya mauwaji ya bodaboda maeneo hayo.

Aidha kamishna huyo amewahakikishia wakaazi wa eneo bunge hilo jipya kuwa usalama utaimarishwa na uchunguzi zaidi unafanywa ili kuwaleta wahalifu katika mikono ya sheria.

BY EDITORIAL DESK