Serikali ya kitaifa imetakiwa kuanzisha mpango wa kuwalipa wazee wa Nyumba Kumi kama njia moja ya kuimarisha hali ya usalama mashinani.
Mwenyekiti wa usalama katika kampuni za kibinafsi Enock Makanga ameitaka serikali kutoa malipo kwa wazee ili kuwapa motisha ya kufanya kazi zao.
Akizungumza katika eneo la Ukunda, Makanga amedai ukosefu wa malipo hayo umewachangia wazee wa Nyumba Kumi kutowajibika kazini.
Wakati uo huo, mwenyekiti huyo ametaja hatua hiyo kama changamoto inayoathiri pakubwa juhudi za kukabiliana na visa vya uhalifu.
Ameitaka serikali ya Kenya kuiga mfano wa mataifa jirani ya Uganda na Rwanda wanaolipa viongozi wa mashinani ili kufanikisha suala la usalama.
BY NEWS DESK