HabariNews

Wawindaji haramu wanaotega wanyama pori katika mbuga ya Shimba Hills wasakwa.

Shirika la kuhifadhi wanyamapori la mbuga ya Shimba Hills KWS kaunti ya Kwale wanawasaka washukiwa wa uwindaji haramu wanaowatega wanyama hao kwenye mbuga hiyo.

Kulingana na naibu wa warden Gilbert Njeru amedokeza kuwa washukiwa hao huaminika kushiriki kwenye biashara za uuzaji wa nyama za wanyama hao jambo alilolitaja kuwa kinyume na sheria.

Aidha afisaa huyo amesema kuwa washukiwa hao wamekuwa wakieka mitego yenye sumu ndani ya mbuga hio kwa lengo la kuwanasa wanyamapori ambao ndio vivutio vikuu vya utalii ambapo kutokana na wanyama hao nchi hupata sarafu za kigeni kupitia wageni wanaozuru mbuga hizo.

Wakati uo huo afisaa huyo asema kuwa idadi ya wanyama iliyokuwepo awali inazidi kurudi chini ikilinganishwa na hapo awali na yote ni kutokana na uwindaji haramu katika mbuga hiyo.

Njeru amewataka wananchi wanaoishi karibu na mbuga hiyo kuchukua tahadhari na kukoma kuendeleza uwindaji na biashara haramu.

Itakumbukwa kwamba ni miezi miwili tu ambapo washukiwa wawili walikamatwa na pembe tano za wanyamapori zenye mizani ya kilo 18 kutoka kijiji cha Vyogato kwenye eneo bunge la Kinango.

BY EDITORIAL TEAM