Bodi ya kitaifa inayosimamia hazina ya CDF nchini imeitaka mahakama ya upeo kufanya maamuzi ya haki katika utata uliozingira hazina hio .
Afisaa mtendaji wa hazina ya CDF nchini Yusuf Mbuno amesema kwamba kufuatia kero la kwamba sheria ya CDF haiambatani na katiba ya nchi, tayari mswada umewasilishwa katika bunge la kitaifa kujadiliwa na kuhakikisha sheria ya CDF inajumuishwa kwenye katiba ili mwelekeo wa utumizi wa hazina hio ufuate sheria za kikatiba.
Mbuno aliyekuwa akizungumza wakati wa kueka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa ya kisasa chini ya CDF katika shule ya msingi ya Burani huko Matuga ameitaja hazina hio kuleta ufanisi mkubwa kwa wananchi hususan wale wanaotoka katika jamii zisizojiweza.
Kwa upande wake mbunge wa Matuga Kassim Tandaza aliye naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hazina ya CDF amewahakikishia wananchi kuhifadhiwa kwa hazina hio kwani mchakato wa kuongeza hazina hio kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 5 unaendelea bungeni.
BY EDITORIAL DESK