Kaunti ya Kilifi inatarajiwa kupokea viwango vya chini vya mvua msimu wa masika, ambao utatanguliwa na mvua za rasharasha zinazotarajiwa kuanza kati ya tarehe 9 na 22 Aprili.
Viwango vya mvua vinatarajiwa kupungua hata zaidi kaunti ya Kilifi msimu huu wa masika ikilinganishwa na mwaka jana.
Kulingana na mkurugenzi wa idara ya hali ya anga kaunti ya Kilifi Geoffery Ogutu, idara hiyo kwa ushirikiano na maofisa wa kilimo tayari imetayarisha warsha yakutoa ushauri kwa wakulima huhusu jinsi wanavyoweza kupata mavuno licha ya kushuhudiwa kwa kiwango kidogo cha mvua.
Amewasihi wakulima wapande mimea inayoweza kustahimili kiangazi kama vile mtama na muhogo ili wasikose mavuno akisistiza kuwa wakulima wengi wamejipata kwenye hali ngumu kutokana na dhana potofu kwamba wakulima wanafaa kupanda mahindi ili kufanikisha kilimo chao.
BY ERICKSON KADZEHA