Wanawake wanaougua ugonjwa wa nasuri huenda wakapata matumaini mapya ya kurejesha hadhi yao katika jamii kufuatia mpango wa matibabu ya bure ya ugonjwa huo kaunti ya Kilifi wiki hii.
Mpango huo unaofanyika kwa ushirkiano wa serikali ya kaunti ya Kilifi na mashirika mbali mbali, unalenga kurejesha hadhi ya wanawake ambao wamekuwa na changamoto ya ugonjwa huu.
Mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake kaunti ya Kilifi Witness Tsuma, anasema mpango huo umekuwa ukiwasaidia wanawake zaidi ya 30 kufanyiwa upasuaji kila mwaka kaunti ya Kilifi, akiwasistiza wanawake kujitokeza zaidi ili kupata usaidizi.
Aidha amewataka wakazi kutopotoshwa na dhana ambazo zimekuwa zikishikiliwa na jamii tangu jadi kuwa ugonjwa wa nasuri ni laana kwa jamii.
Ametoa wito kwa jamii kukoma kuwanyanyapaa wanawake wanaougua nasuri, akisema ni ukiukaji wa haki ya wagonjwa hao.
BY ERICKSON KADZEHA