Wakaazi na waekezaji waliojenga kandokando mwa ufuo za bahari wametakiwa kuchukua tahadhari ya mmomonyoko wa ardhi (land slides)msimu huu wa mvua kwa usalama wao.
Kulingana na mkurugenzi wa halmashauri ya mazingira nchini Nema tawi la Kwale Godfrey Wafula baadhi ya wakaazi wamejenga kwenye hifadhi ya fuo ya bahari ambayo msimu huu wa mvua sio salama kufuatia kasi ya mawimbi .
Amewataka wakaazi kuhakikisha wanajenga kwa kufuata sheria ya kujenga mita 60 kutoka kwa fuo ya bahari kwa usalama wao.
BY EDITORIAL DESK