Changamoto imetolewa kwa Serikali ya kitaifa kupitia kwa halmashauri ya bandari kutatua changamoto ya msongamao katika kivuko cha likoni Ferry.
Gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema kuna haja kwa serikali kuu kushirikiana na viongozi katika halmashauri ya bandari ya Mombasa kushughulikia suala hilo ili kuwapunguzia dhiki watumizi wa kivuko hicho.
Akizungumza baada ya ibada ya Jumapili katika eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale Achani amedai kuwa msongamano huo unalemaza sekta ya utalii kwani watalii wengi wanaotumia kivuko hicho hupoteza muda mwingi kabla ya kuvuka.
“Pia ningekuomba mheshimiwa Rais feri! feri !feri! Mheshimiwa yatutesa sisi watu wa Kwale, watalii wetu wamekuwa na kibarua kigumu wanakaa 5hrs kwa kivuko kungoja kuvuka watalii wetu wanakataa kuja Kwale kwa sababu ya Kenya Ferry,” amesema Achani.
Vilevile Achani amesisistiza kuwa viongozi katika kaunti ya Kwale wamesimama kidete na kuungana kuhakikisha amani inadumishwa huku akiwakemea vikali vikali wanaojaribu kuvuruga amani wakitumia kisingizio cha maandamano ili kuzua rabsha na fujo katika kaunti hiyo.
BY EDITORIAL DESK