Mbunge wa Kinango Gonzi Rai amemsihii Rais Wiliam Ruto kupitia serikali yake kuwapa nafasi za ajira katika idara ya utawala jamii kutoka kaunti yak wale ambayo ina idadi chache katika idara hiyo.
Gonzi akizungumza katika kaunti ya kwale wakati wa ziara ya siku tano ukanda wa pwani, ameeleza kusikitishwa kutokana na idadi chache ya jamii ya kwale kuwepo katika idara ya utawala.
Aidha amemtaka Ruto kuzingatia kilio chao kama wakazi wa kwale ili kunga mianya hiyo,
Kiongozi huyo aidha amemuomba rais Ruto kando na nyadhfa katika ngazi za utawala, jamii hiyo kadhalika kuweza kupata nafasi katika uteuzi unaoendelea serikalini.
Baadhi ya wakereketwa wa kisiasa hapa Pwani wanahisi kwamba ziara Rais William Ruto Pwani, haikumwanagazia mwananchi wa kawaida badala yake uharibifu wa mali ya serikali.
Akizungumza na meza yetu ya habari mkereketwa wa kisiasa kaunti ya Mombasa Millicent Odhiamabo, amesema viongozi waliokuwa katika ziara hiyo hawakusisitiza kuhusu maswala ya mwanainchi kama vile gharama ya maisha.
Akitolea mfano hatua ya rais kutoa hundu kwa wavuvi ukanda wa Pwani Odhiambo, amesema pesa hizo hazitamfaidi yule mvuvi aliye na njaa kubwa badala yake angemwezesha kupitia mafunzo ya kujiendeleza.
Wakati huo huo Odhiambo ameongeza kuwa huenda mazungumzo baina ya serikali na upinzani yasiwe na faida yoyote kwa mkenya akisema masharti yaliyowekwa hayawezi kufaulu.
Mwanasiasa huyo kadhalika amedokeza kuwa baadhi ya viongozi wa Kanya Kwanza wamekuwa vizuzizi vya mazungumzo hayo kutofanyika akitishia kwamba huenda mrengo wa Azimio ukasalia kwenye maandamano hadi pale serikali itaskiza kilio cha mwanainchi wa kawaida.
Millicent amerai serikali ya Kenya Kwanza kushusha ushuru unaotozwa mwanainchi kama njia moja ya kumwezesha mwanainchi kujimudu kimaisha.
BY EDITORIAL DESK